Kamanda wa Hezbollah, auawa Damascus

Haki miliki ya picha AP
Image caption Samir Qantar

Watu watiifu kwa serikali ya Syria na kundi moja la wapiganaji nchini Lebanon la Hezbollah, wamesema kuwa kinara mkuu wa kundi hilo ameuwawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Israeli mjini Damascus.

Wanasema kuwa Samir Qantar aliuwawa na roketi lililopiga jumba alimokuwa akiishi katika wilaya ya Jaramana.

Alihukumiwa jela maisha nchini Israeli mnamo mwaka wa 1979 akituhumiwa kutekeleza shambulio nchini Israeli lililowauwa watu wanne.

Image caption Aliwahi kuhukumiwa jela maisha nchini Israeli mnamo mwaka wa 1979

Aliachiliwa huru miaka saba iliyopita katika hatua ya kubadilishana wafungwa wanajeshi wa Israel waliokuwa wamekamatwa na kundi la Hezbollah mwaka 2006.

Waziri mmoja wa Israeli amefurahia kifo chake, lakini hajasema ikiwa Israel ilihusika katika kuuliwa kwake.