Mazungumzo Yemen yavunjika

Image caption Mazungumzo ya amani Yemen

Mazungumzo ya kutafuta amani na kusitisha vita vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen yamevunjika, kwa makubaliano tu kuendelea tena mwanzoni mwa mwaka ujao.

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa, Ismail Ould Cheikh Ahmed, katika mkutano na waandishi habari nchini Switzerland amenuuliwa akisema kwamba mazungumzo yamekuwa na mafanikio.

Pande hizo mbili zimejadiliana masuala kadhaa ikiwemo, upatikanaji wa mashirika ya misaada, ubadilishanaji wafungwa na uondoaji wa makundi ya waasi pamoja na silaha. Mwandishi wa BBC amsema kwamba umoja wa mataifa unaamini kwamba maendeleo zaidi yatategemea usitishwaji mapigano.

Mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miezi 9 yamesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu sita.vita hivyo vimesababisha nchi jirani ya Yemen kuwa mashakani na wakati huo huo Saudi Arabia kuingilia kati mzozo huo huku ikijaribu kutaka kumrejesha madarakani rais Abdrabbuh Mansour Hadi. Rais huyo awali aling'olewa madarakani na waasi wa madhehebu ya Shia wa Houthi ambao ni washirika wa Iran.