Marekani yashambuliwa Afghanistan

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga huko nchini Afghanistan amewaua askari sita wa vikosi vya jeshi la Marekani miongoni mwa shambulio baya kuwahi kutokea miezi ya hivi karibuni.

Mshambuliaji huyo akiwa kwenye pikipiki, aliwalenga askari wa vikosi vya muungano kati ya majeshi ya NATO na askari wa doria wa Afghanistan karibu na kambi ya vikosi vya anga. Taliban wamekiri kufanya shambulio hilo.

Pamoja na mauaji hayo kukera yaliyofanywa upande wa mkoa wa kusini wa Helmand; Wapiganaji wanasema wameweza kuchukua udhibiti wa wilaya ya Sangin.

Kamanda wa polisi ameiambia BBC kwamba yeye na wasaidizi wake pamoja na kikosi cha askari walizingirwa na kutawanyika katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo .

Mamia kadhaa wa vikosi vya usalama vya Afghanistan wameuawa katika eneo hilo la Helmand mwaka huu.