Malawi imefuta hukumu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Image caption Malawi imefuta hukumu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Utawala nchini Malawi umewaondolea mashtaka wanaume wawili waliofumaniwa wakishiriki mapenzi ya jinsia moja, baada ya Uingereza na Marekani kuingilia kati.

Waziri wa sheria nchini Malawi, Samuel Tembenu amesema kuwa mashtaka dhidi yao yameondolewa.

Raia wa Malawi Cuthbert Kulemela na Kelvin Gonani walitiwa mbaroni, na wakahukumiwa na kuzuiliwa kwa muda wa wiki mbili zilizopita, kwa tuhuma za kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Lakini baada ya Marekani na Uingereza kuingilia kati , kwa kuangazia ukikwaji wa haki za binadamu nchini humo, kwa kutumia mitandao ya kijamii na maswali bungeni, mamlaka nchini Malawi imetupilia mbali maashtaka dhidi ya wawili hao.

Waziri wa sheria Samwel Tembenu amesema kuwa mashtaka yao yameondolewa.

Na si hayo tu alisema Malawi inasitisha kwa muda hukumu dhidi yao, wakisubiri matokeo ya sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, ambazo wengi wanasema zimepitwa na wakati.

Mamlaka nchini Uingereza haijathibitisha iwapo ilitishia kusitisha msaada wa pauni 400 inazoipa Malawi kila mwaka.

Malawi imekuwa ikiangaziwa sana kwa msimamo wake mkali kuhusu sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Awali wanasiasa kutoka Malawi waliikemea baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, kwa kile walisema ni kuwasukumia swala la mahusiano ya jinsia moja.