UN: Boko Haram imesababisha milioni kutoroka shuleni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption UN: Boko Haram imesababisha milioni kutoroka shuleni

Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto UNICEF, linasema kuwa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria na kwenye nchi zingine yamewalazimu zaidi ya watoto milioni moja kuacha masomo.

Katika ripoti mpya, UNICEF inasema kuwa mamia ya shule zimeshambuliwa , kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mzozo huo ambao umedumua kwa kipindi cha miaka sita.

Image caption Shule nyingi katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria zimegeuka kuwa kambi za wakimbizi.

Nchini Nigeria kwenyewe wanamgambo hao waliwaua karibu walimu 600.

Katika taifa jirani la Cameroon ni moja tu kati ya shule 100 zilizofungwa mwaka uliopita ambayo imefunguliwa.

Umoja wa mataifa una hofu kuwa huenda watoto hao wakaacha kwenda shule kabisa katika maeneo hayo.

Image caption Kufikia sasa watu 17,000 wameuawa huku takriban wakaazi milioni 2 wakilazimika kutoroka makwao.

Licha ya amri ya rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buharikwa makamanda wake wa jeshi kuzima mashambulizi ya Boko Haram ,kundi hilo bado linaendelea kuwaua watu katika ukanda wa Magharibi mwa Afrika.

Kufikia sasa watu 17,000 wameuawa huku takriban wakaazi milioni 2 wakilazimika kutoroka makwao.

Shule nyingi katika maeneo ya Kaskazini mwa Nigeria zimegeuka kuwa kambi za wakimbizi.

Image caption UNICEF inasema kuwa mamia ya shule zimeshambuliwa , kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mzozo huo ambao umedumua kwa kipindi cha miaka sita.

Boko Haram ambayo ni tafsriri ya ''elimu ya kisasa ni haramu'' imekuwa ikilenga shule nchini Nigeria kwa hofu watoto walioelimika hawafuati masharti na kanuni za dini ya Kiislmu.

Mwaka uliopita kundi hilo liligonga vichwa vya habari kote duniani baada ya kuwateka nyara wanafunzi 200 wa kike katika mji wa Chibok.

Hadi kufikia sasa wasichana hao wanafunzi hawajulikani waliko.