Iraq yazingira Islamic State mjini Ramadi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa Iraq wanasema kuwa wameteka maeneo mengi ya mji wa Ramadi

Mamlaka nchini Iraq inasema kuwa vikosi vya serikali vimeanzisha mashambulizi makali ya kukomboa eneo la katikati mwa mji wa Ramadi, ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Islamic State tangu mwezi wa Mei.

Maafisa wa Iraq wanasema kuwa vikosi vya serikali vikiungwa mkono na vikosi vya kikabila pamoja na mashambulizi ya angani kutoka kwa vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani, vimefanikiwa tangu mwanzo wa mashambulizi hayo yalioanza usiku wa manane.

Serikali ya Iraq imefanya ukombozi wa mji wa Ramadi kuwa lengo kuu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Iraq yazingira Islamic State mjini Ramadi

Imekuwa ikijitayarisha kwa miezi kadha, kukata njia za usambazaji wa bidhaa, na mara kwa mara, kuwataka wenyeji mjini humo kuhama.

Swala hilo limekuwa kikwazo kikuu, kwani watu wengi wamesalia mjini humo, na kutatiza mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na vikosi vya muungano .

Inakadiriwa kuwa mamia ya wapiganaji wa Islamic State wamesalia Ramadi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa Iraq wanasema kuwa vikosi vya serikali vinaungwa mkono na vikosi vya kikabila

Ripoti kutoka huko zinasema wamekuwa wakijaribu kutuliza uasi dhidi yao, na pia kuwazuia raia kuondoka.

Mamalaka nchini Iraq inasema kuwa vikosi vya kikabila vimejiunga na mashambulizi ya kukomboa mji huo, na kusema kuwa huenda wakaukomboa mji huo ifikapo mwishoni mwa wiki hii.