Mali yatangaza siku 10 ya hali ya tahadhari

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mali yatangaza siku 10 ya hali ya tahadhari

Serikali nchini Mali imetangaza siku 10 za hali ya tahadhari kutokana na hofu ya utovu wa usalama haswa wakati huu wa likizo ya kufunga mwaka .

Taarifa kutoka kwa serikali inasema kuwa hatua hiyo itawapa maafisa wa usalama nguvu zaidi wakati wa kushika doria msimu huu wa likizo.

Mwezi Novemba wapiganaji wa kiislamu wa al-Murabitoun walishambulia hoteli moja mjini Bamako, na kuwauwa watu 20, wengi wao wakiwa raia wa kigeni.