Michel Platini aitupia lawama FIFA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michel platini

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya, Michel Platini ameitupia lawama kamati ya nidhamu shirikisho la soka Duniani FIFA,na kusema kuwa walikuwa wanalala usingizi kwa Zaidi ya miaka 4 kabla ya kumzuia kujishughulisha na soka.

Platin na Rais wa FIFA Sepp Blatter waliamriwa kuondoka madarakani kutokana na kashifa inayowakabili na kuwazuia kujishughulisha na masuala ya soka miaka.

Viongozi hao wa juu Blatter na Platin wanatarajiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliochukuliwa dhidi yao. Wote wawili wanakata rufaa kupinga hjatua hiyo ya kufungiwa kwao.

Hata hivyo katika mahojiano maalumu na shirika la habari la AFP Platini amesema anatarajia kuwania uchaguzi ujao mwezi Februari na anauhakika wa kushinda