Davies ajiuzulu kupisha uchunguzi

Image caption Nick Davies,astaafu kwa muda kupisha uchunguzi,dhidi ya sakata la Urusi.

Afisa mwandamizi katika mchezo wa riadha Duniani Nick Davies ameamua kujiuzuru kwa muda kupisha uchunguzi wa ndani kufuatia sakata la barua pepe iliyotumwa inayohusishwa na kashfa ya Urusi kuhusiana na udanganyifu michezoni.

Barua pepe hiyo ya taasisi hiyo ya mchezo wa riadha inadaiwa inadaiwa kucheleweshwa makusudi kutoa orodha ya kutoa orodha ya wanamichezo kutoka Urusi wanaotuhumiwa kwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni ili kuepusha usumbufu kuelekea mashindano ya Dunia ya riadha mwaka 2013 huko Moscow.

Davies amekanusha kuhusika na tuhuma hizo na kwamba wajibu wake ilikuwa ni kusimamia nidhamu ya taasisi hiyo.

Hata hivyo wakati barua pepe hiyo ikiandikwa kulikuwa na tuhuma dhidi ya Urusi kuhusiana kutokana na udanganyifu michezoni na majadiliano kuhusiana na uhalali wa Urusi kuendelea kuandaa mashindano hayo.