Wapenzi wa jinsia moja kutoa damu baada ya mwaka 1

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wapenzi wa jinsia moja kutoa damu baada ya mwaka 1

Serikali ya Marekani imebatilisha marufuku yake ya miaka 30 kuwazuia wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kutoa damu.

Sheria hiyo iliwekwa mwaka 1983 wakati visa vya ugonjwa wa ukimwi vilianza kuibuka.

Shirika linalohusika na chakula na madawa nchini Marekani linasema kuwa 'wanaume hao' wataruhusiwa kutoa damu ikiwa hawajafanya mapenzi kwa muda wa mwaka mmoja !

Baadhi ya watatezi wa haki za wapenzi ya jinsia moja wanasema kuwa sheria hizo mpya bado ni za kibaguzi.

Image caption Wanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja wanadai kuwa sheria bado zinawabagua.

Wanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja wanadai kuwa sheria bado zinawabagua.

Wanasema kuwa njia za kisasa za kipima virusi vya ukimwi zinamwezesha mtu kupimwa na kutoa damu kwa muda mfupi.