Taliban wakamata wanajeshi - Afghanistan

Image caption vikosi vya Uingereza kilichokuwa Afghanstan kikiondoka Sangin

Kikosi kidogo cha majeshi ya serikali ya Afghanistan kinaripotiwa kushikiliwa katika kambi ya kijeshi upande wa kusini mwa nchi hiyo, na kuzingirwa na vikosi vya wanamgambo wa Taliban.

Vikosi vya wanamgambo wa Taliban vinasemekana kukamata eneo lote la Sangin katika jimbo la Helmand,na kuteketeza kituo cha polisi katika eneo hilo na pia kusambaratisha makao makuu ya serikali Jumatano wiki hii.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wamenyongwa hadi kufa. Naye gavana wa wa Sangin alichukuliwa kwa usafiri wa anga na kuondolewa mjini humo.

Inaarifiwa pia kwamba majeshi ya serikali yamewasili katika eneo hilo ingawa bado hawajafanikiwa kuingia katika eneo hilo la Sangin. Na shughuli ya kuukomboa mji huo bado inaendelea.