Mbwa pia wajua kuonyesha hisia

Image caption Je wajua kuwa mbwa nao wanajua kuigiza hisia ?

Mbwa wanaweza kuonyesha hisia zao kwa haraka kama wanadamu na kuonyesha ishara za huruma!

Haya ni kulingana na wachunguzi wa kutoka Utaliano.

Kuiga onyesho la uso mwingine ni tabia ya mwanadamu inayowasaidia watu kuelewana.

Kwenye jarida la Royal Society Open Science, wanasayansi wamesema kuwa, mbwa nao wanaweza kufanya hivyo kutangamana na mbwa wengine.

Wanafikiria kuwa mbwa wanaweza kuonyesha huruma ya kawaida unaowawezesha kufahamu hisia.

Image caption Baada ya kutathmini video kwa saa 50, walipata kuwa mbwa walikuwa wanaigana.

Pia wanasayansi wameongezaa kuwa wamefanya ufumbuzi huo walipokuwa wanawapa mafunzo mbwa.

‘’Tumeonyesha kuwa mwigo upo pia kwenye mbwa na ni kawaida, kwa hiari.

'Vilevile uigizaji haraka wa mbwa wengine.'' Mwanasayansi Dr Elisabetta Palagi ameiambia BBC.’’

Mbwa pia wametambulika kuwa na utu kutokana na kuonyesha ishara za huruma kwa mbwa wengine wanapoonyesha dalili tofati kwa ishara ya uso.

"Mbwa pia anapocheza na mbwa mwenzake, anaweza kufahamu motisha yake na hisia zake kwa kumuiga," Dr Palagi alifafanua

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kuiga onyesho la uso mwingine ni tabia ya mwanadamu inayowasaidia watu kuelewana.

Wanasayansi watatu waliokuwa wanafanya kazi na kitengo cha wanyama wa hali ya juu mjini Rome walichukua video za mbwa wakicheza mjini Palermo, Utaliano.

Walitathmini jinsi mbwa walivyokuwa wanatangamana pamoja na ishara za kunyesha mbwa anapocheza kama vile, kuegemea miguu yake ya mbele na kufungua mdomo.

Baada ya kutathmini video kwa saa 50, walipata kuwa mbwa walikuwa wanaigana.

Wanasayansi hao wa Utaliano wanapanga kuchunguza mbwa mwitu kueleza zaidi uhusiano kati ya wanadamu na mbwa.