Colombia imehalalisha bangi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Colombia ,Juan Manuel Santos, ametia sahihi sheria mpya inayohalalisha matumizi ya bangi

Rais wa Colombia , Juan Manuel Santos, ametia sahihi sheria mpya inayohalalisha matumizi ya bangi kwa manufaa ya kimatibabu

Katika hotuba kwa taifa kupitia kwa runing bwana Santos alisema kuwa sheria hii kimsingi inaiweka Colombia katika mtsari wa mbele wa kupamabana na matumizi ulanguzi na ukuzaji wa bangi Kusini mwa Marekani.

"Tumechukua hatua ya kwanza kuisadia Colombia kupambana na gonjwa hili sugu la matumizi ya mihadarati.

Sheria hii itasaidia kufaidi kile kinachoitwa kuwa uwezo wa kimatibabu ya mmea huu ;bangi.''alisema rais Manuel Santos.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hata hivyo alisisitiza kuwa sheria hii mpya haikinzani hata kidogo na mswada wake wa kupambana na mihadarati.

Hata hivyo alisisitiza kuwa sheria hii mpya haikinzani hata kidogo na mswada wake wa kupambana na mihadarati.

" kufaidi uwezo wa utabibu wa bangi kwa hakika haizuii kwa vyovyote msimamo wetu dhabiti wa kupambana na matumizi ya mihadarati.''

Tutaendelea mbele na harakati za kupambana na ulanguzi wa madawa mengine haramu alisema rais Manuel Santos.

"Sheria hiyo mpya inaruhusu ukuzaji wa mmea huo kwa wale tu waliopewa idhini na serikali''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Colombia imekuwa mshiriki mkubwa wa serikali ya Marekani katika mikakati yake ya kupambana dhidi ya ulanguzi na ukuzaji wa mihadarati.

Colombia imekuwa mshiriki mkubwa wa serikali ya Marekani katika mikakati yake ya kupambana dhidi ya ulanguzi na ukuzaji wa mihadarati.

Taifa hilo limefaidi mabilioni ya dola katika misaada mbali na kutumia jeshi lake katika vita dhidi ya magenge ya walanguzi.

Santos alitangaza sheria hiyo mpya miezi michache tu baada yake kupiga marufuku upulizaji wa madawa ya Monsanto baada ya shirika la afya duniani WHO kusema kuwa utafiti umeonesha kuwa Roundup inasababisha saratani.