Waandamana kupinga mauaji ya mweusi Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamana kupinga mauaji ya mweusi Marekani

Kundi linaloteta haki za binadamu na haswa uswa wa kijamii nchini Marekani 'Black Lives Matter' limeandaa maandamano na kufunga viwanja viwili vya ndege na duka kubwa zaidi la jumla nchini humo.

Waandamanaji wawili walikamatwa kwenye duka hilo lililo katika mji wa Minneapolis wakati polisi walikuwa wakivunja maandamano yanayotaka kuwepo haki kwa Jamar Clark, mwanamme mweusi ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini humo mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waandamanaji 15 wakamatwa

Maandamano mengine yalifunga kwa muda barabara zinazoingia uwanja wa ndege yakiwa sawa na maandamano yaliyofanyika mjini San Francisco.

Taarifa kwenye akaunti ya mtandao wa facebook wa kundi hilo ilisema kuwa hali haitakuwa ya kawaida hadi kutakapokuwa haki kwa waliouawa na wale walio hai.