Makabiliano makali yazuka West Bank

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Makabiliano makali yazuka West Bank

Kumetokea mashambulizi kadhaa yanayotekelezwa na Wapalestina dhidi ya Waisraeli katika eneo linalozozaniwa la West Bank.

Makabiliano hayo yanachacha wakati ambapo maelfu ya watalii wamekusanyika kwa sherehe za mkesha krismasi.

Katika shambulizi moja, walinzi wawili walidungwa kisu katika eneo la wayahudi, huku mpalestina mwingine akijarubu kuwavamia wanajeshi kwa kutumia bisibisi .

Kwenye kisa cha tatu, mwanamme mmoja alijaribu kuwagonga wanajeshi kwa kutumia gari kwenye kambi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanaume wote watatu wapalestina waliuwawa.

Wanaume wote watatu wapalestina waliuwawa.

Usalama umeimarishwa wakati ambapo mji wa Bethlehem unajiandaa kuwapokea waumini wa kikristo wakati wa sherehe za krismasi katika kanisa moja lililoko mahali panapoaminika, kuwa ndipo yesu alikozaliwa.