Cameroon haijaelezea waliko washukiwa 130

Image caption Cameroon haijaelezea waliko washukiwa 130

Shirika la Amnesty International, limeomba mamlaka kuu nchini Cameroon, kuelezea hatma ya watu 130 waliokamatwa wakati wa operesheni dhidi ya kundi moja la wapiganaji wa kiislamu wa, Boko Haram, mwaka mmoja uliopita.

Katika taarifa ya kundi hilo iliyotolewa katika maadhimisho ya kwanza ya mwaka mmoja tangu kutoweka kwao, shirika hilo la kutetea haki za binadamu, linasema kwamba wanaume na wavulana 200 walizuiliwa katika vijiji vya Magdeme na Double kaskazini mwa Cameroon.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali ilisema baadaye kuwa imewakamata wanamgambo 70

Serikali ilisema baadaye kuwa imewakamata wanamgambo 70 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram -- lakini hakuna taarifa zozote kuwahusu watu wengine waliozuiliwa.

Awali serikali ya Camroon, ilikanusha madai ya kuwatesa na hatimaye kuwauwa washukiwa hao.