Mmiliki wa timbo iliyoporomoka China ajiua

Haki miliki ya picha Xinhua
Image caption Mmiliki wa timbo iliyoporoka China ajiua

Shirika kuu la habari la serikali nchini China, limetangaza kuwa mmiliki wa migodi ya madini aina ya jasi iliyoko Mashariki mwa jimbo la Shandong nchini Uchina amepatikana amejitia kitanzi.

Shirika la habari la taifa la Xinhua linaripoti kuwa Ma Congbo, mwenyekiti wa kampuni iliyomiliki mgodi huo wa Yurong ulioporomoka, amepatikana amekufa maji katika moja ya vidimbwi vinavyotumika na kam[uni yake kuhifadhi maji.

Ma amepatikana ameaga dunia siku mbili tu baada ya maporomoko ya ardhi kutokea katika eneo la kuhifadhia mabaki ya ujenzi na jaa la mchanga unaotolewa katika timbo hilo katika mkoa wa Shandong.

Bado makundi ya waokoaji yanajaribu kuwafikia wachimbaji migodi kumi na saba ambao wamekwama chini ya ardhi kwa siku ya pili sasa.

Baadhi yao wameokolewa huku maiti moja ikipatikana.

Haki miliki ya picha Xinhua
Image caption Shirika la habari la taifa la Xinhua linaripoti kuwa Ma Congbo, amepatikana amekufa maji

Wachimbaji migodi hao wanachimba jasi ambayo ni aina ya rasilimali inayotumika katika ujenzi.

Zaidi ya watu 900 walifariki katika mkasa wa kuporomoka kwa migodi nchini Uchina mwaka jana.