Jeshi la Iraq latwaa ngome ya IS Ramadi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jeshi la Iraq latwaa ngome ya IS Ramadi

Chanzo kimoja cha habari kutoka jeshi la Iraq kimesema wanajeshi wa jeshi la Iraq wanazidi kusogea kwenye jengo la makao makuu ya mji wa Ramadi ambalo hadi sasa lingali mikononi mwa kundi la wapiganaji wa ISIS.

Haki miliki ya picha AP
Image caption wapiganaji wa kundi la ISIS walionekana kusalimu amri na kuondoka wenyewe kwenye makao makuu ya mji wa Ramadi

Chanzo cha habari cha jeshi kinasema wapiganaji wa kundi la ISIS walionekana kusalimu amri na kuondoka wenyewe kwenye makao makuu ya mji wa Ramadi ambalo ni eneo muhimu katika mapigano ya wiki nzima ya jeshi la Iraq na wanamgambo hao.

Wapiganaji hao wamekuwa wakiutumia eneo hilo kupanga mashambulizi yao dhidi ya jeshi la Iraq katika kupigania kutawala mji huo.

Jeshi limeingia kwenye moja ya majengo ya ofisi hizo lakini wamekuwa na wasiwasi huenda wapiganaji wa ISIS wameweka mabomu ya kutegesha kuzunguka majumba hayo.

Image caption Mwandishi wa BBC anasema hali inayoendelea kwa sasa inaonyesha jeshi la Iraq linakaribia kuukomboa mji huo wa Ramadi

Mwandishi wa BBC anasema hali inayoendelea kwa sasa inaonyesha jeshi la Iraq linakaribia kuukomboa mji huo wa Ramadi ambao ulinyakuliwa na wanagambo hao wa ISIS mapema mwaka huu katika kisa kilichokuwa pigo kubwa kwa serikali ya Iraq.