Mafuriko makubwa zaidi katika miaka 50 Marekani Kusini

Image caption Mataifa yaliyoathirika ni pamoja na Paraguay, Argentina, Brazil na Uruguay.

Kimbunga kimepiga jimbo la Texas nchini Marekani na kuezua mapaa ya nyumba, kuharibu magari na kufanya baadhi ya maeneo ya mji wa Dallas kubakia katika giza totoro.

Angalau watu 26 mpaka sasa wanasemekana kupoteza maisha katika tukio hilo ambalo limeyakumba maeneo mengi ya Kusini mwa Marekani katika siku za karibuni.

Hali mbaya ya hewa imeathiri eneo kubwa la Marekani kusini katika msimu huu wa Krismasi, na kusababisha vifo vya watu 26.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mvua iliyonyesha mfululizo kwa siku kadhaa, imesababisha mito kufurika kupita kiasi

Mataifa yaliyoathirika ni pamoja na Paraguay, Argentina, Brazil na Uruguay.

Mvua iliyonyesha mfululizo kwa siku kadhaa, imesababisha mito kufurika kupita kiasi, hasa katika maeneo tambarare ya nyanda za chini.

Wengi wa watu waliolazimika kimbilia usalama wao wanatoka katika maeneo ya mpakani katika mji wa Concordia, mahali ambapo viwango vya maji ya mto Uruguay, vimeongezeka maradufu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Upepo mkali umeharibu nyaya za umeme, na kusababisha ukosefu mkubwa wa nguvu za umeme

Nchini Paraguay, taifa ambalo limeathirika zaidi, wakuu wanasema kuwa viwango vya maji vinaendelea kufurika.

Upepo mkali umeharibu nyaya za umeme, na kusababisha ukosefu mkubwa wa nguvu za umeme katika mji mkuu Asuncion, na maeneo mengine ya jirani.

Rais Mauricio Macri, atazuru eneo hilo hatimaye leo Jumapili.