Rais mpya wa Burkina Faso ameapishwa

Haki miliki ya picha
Image caption Rais mpya wa Burkina Faso kuapishwa leo

Aliyekuwa waziri mkuu wa Burkina Faso Roch Mark Christian Kabore, ameapishwa kuwa rais nchi hiyo .

Rais Christian Kaboré aliwaambia maelfu ya raia walikusanyika katika bustani ya mji mkuu wa Ouagadougou "Naapa kuwatumikia watu wa Burkina Faso kwa uadilifu na kujitolea kwa roho moja ''

Alishangiliwa na wageni na wenyeji.

''Nitahakikisha kuwa nitatekeleza na kuilinda katiba ya nchi na sheria za Burkina Faso.''

''Nitahakikisha usawa kwa watu wote wenye asili ya Burkina Faso''

Bwana Kabore ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita, alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani Blaise Compaore.

Image caption Viongozi wa mataifa 5 ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake.

Compaore alinyakua mamlaka baada ya mapinduzi ya kijeshi, na kutawala taifa hilo kwa miaka 27 hadi mapinduzi yaliyofuatia maasi makubwa ya umma mwaka uliopita.

Kabore alitofautiana na Compaore mwaka uliopita alipotangaza nia ya kuendelea kuongoza.

Viongozi wa mataifa 5 ya Afrika walihudhuria hafla ya kuapishwa kwake.

Tangu ijinyakulie uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1960, asilimia kubwa ya viongozi wa Burkina Faso wamekuwa wakijinyakulia uongozi kwa mtutu wa bunduki.