WHO yasema Guinea haina Ebola

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mgonjwa wa mwisho wa Ebola Guinea

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa Guinea haina tena maambukizo ya ugonjwa wa Ebola.

Mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Ebola ulianza nchini humo miaka miwili iliyopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watoto 6,220 wameachwa yatima kwa kupoteza mzazi mmoja ama wote wawili kutokana na ugonjwa huo

Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi za Afrika magharibi, hususan katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Waguinea wanajiandaa kusherehekea kumalizika kwa janga hilo nchini mwao kwa kufanya maonesho na kurusha fataki.

Wengi wanasema wanaanza mwanzo mpya na mwaka mpya na pia kwa rais wao Alpha Conde ambaye muhula wake wa uongozi ulianza wiki iliyopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtoto wa mwezi mmoja ndiye aliyekuwa mgonjwa wa mwisho wa Ebola kutibiwa

Hata hivyo ugonjwa wa Ebola umeweka kumbukumbu mbaya nchini humo, hususan athari za kijamii na kiuchumi.

Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, nchini humo watoto 6,220 wameachwa yatima kwa kupoteza mzazi mmoja ama wote wawili kutokana na ugonjwa huo.

Wale walioathiriwa na ugonjwa huo, pia bado wanaishi kwa hali ya mashaka na kubaguliuwa.