Kiongozi wa zamani Israel Ehud Olmert kufungwa jela

Ehud Haki miliki ya picha AP
Image caption Olmert alikuwa waziri mkuu kati ya 2006 na 2009

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ehud Olmert ametakiwa kutumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa makosa ya rushwa.

Olmert alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na mahakama ya chini 2014, lakini adhabu hiyo sasa imepunguzwa na Mahakama ya Juu.

Mwanasiasa huyo wa umri wa miaka 70 alipatikana na hatia kuhusu mkataba wa ujenzi wa nyumba ambao ulifanyika alipokuwa meya wa Jerusalem, kabla yake kuwa waziri mkuu 2006.

Olmert, aliyejizulu 2009, atakuwa waziri mkuu wa kwanza wa zamani wa Israel kwenda gerezani.

Pia amekata rufaa uamuzi wa kumpata na hatia ya utapeli na kuvunja kanuni ya uaminifu.