Bill Cosby ashtakiwa dhuluma ya kimapenzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bill Cosby ashtakiwa kwa dhulma ya kimapenzi

Waendesha mashtaka katika jimbo la Pennsylvania Marekani wamemfungulia mashtaka ya kwanza mcheshi nguli Bill Cosby .

Cosby ameshtakiwa kwa makosa ya dhuluma za kimapenzi dhidi ya mfanyikazi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Marekani.

Kosa hilo yamkini lilifanyika mwaka wa 2004.

Cosby amekana madai yeyote dhidi yake na hata amewafunguliwa mashtaka wanawake anaodai wanalenga kumpunja pesa.

Awali mchekeshaji huyo alikana kuwadhulumu kimapenzi akijitetea kuwa aliwahi kushiriki mapenzi baada ya kukubaliana na wanawake hao.

Mashtaka dhidi yake yalifufuliwa baada ya idadi kubwa ya wanawake kuibuka wakidai walipewa dawa na kisha kudhulumiwa kimapenzi na mchekeshaji huyo nguli.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cosby amekiri kutumia dawa hizo za Quaaludes.

Bi Andrea Constand, aliyekuwa mfanyikazi wa chuo kikuu cha Temple ndiye aliyemshtaki Cosby mara ya kwanza mwaka wa 2005

Uchunguzi ulibaini kuwa bwana Cosby alikuwa akiwapa wahasiriwa dawa aina ya Quaaludesinawalegeza na hat wengine wanasinzia kabla ya kushiriki mapenzi nao.

Cosby amekiri kutumia dawa hizo za Quaaludes.