Kiongozi wa IS aliyehusishwa na mauaji Paris auawa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Charaffe al Mouadan

Kiongozi wa kundi la Islamic State ambaye amehusishwa na shambulio la kigaidi la Paris Ufaransa ameuawa na majeshi ya muungano.

Jeshi la Marekani limesema kiongozi huyo Charaffe al Mouadan alikufa katika katika shambulio la kutoka angani.

Msemaji wa jeshi la Marekani amesema mpiganaji huyo wa Kisyria alikuwa akipanga mashambulizi zaidi dhidi ya nchi za magharibi na alikuwa na mawasiliano ya karibu na anayetuhumiwa kupanga shambulio la Paris.

Jeshi la Marekani limesema viongozi 10 wa Islamic State wameuawa mwezi huu.