Msaidizi wa rais wa Korea Kaskazini afariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msaidizi wa ngazi ya juu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amefariki dunia.

Msaidizi wa ngazi ya juu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amefariki dunia.

Kim Yang - Gon , 73, alifariki katika ajali ya barabarani , shirika la habari la KCNA limesema.

Gon , alikuwa katibu wa chama tawala cha wafanyakazi na alikuwa msimamizi wa mahusiano na Korea ya Kusini .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Yang - Gon , 73, alifariki katika ajali ya barabarani , shirika la habari la KCNA limesema.

Yeye ni mmoja wa viongozi wa juu waliokuwa kwenye ujumbe kutoka Korea ya Kaskazini ambao wamesaidia kupunguza uhasama baina ya mataifa hayo mawili hususan baada ya kufyatuliana makombora mapema mwezi Agosti.

Shirika la habari la serikali limemtaja kama "rafiki wa karibu na imara'' wa rais Kim Jong-un .

Kim Jong-un akiandamana na wanachama wakuu wa serikali yake 80- watahudhuria mazishi ya bwana Kim siku ya Alhamisi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gon , alikuwa katibu wa chama tawala cha wafanyakazi na alikuwa msimamizi wa mahusiano na Korea ya Kusini .

Mvutano kati ya Kaskazini na Korea ya Kusini uliongezeka mwezi Agosti wakati mlipuko uliotokea mpakani kujeruhiwa maafisa 2 wa Korea Kusini.

Mikutano ya mapatano wakati huo ilisababisha nchi hizo mbili kuepuka mapambano ya kijeshi.