Sili asababisha foleni ndefu Marekani

Image caption Sili asababisha foleni ndefu California

Wakaazi wa mji wa California walilazimika kutafuta njia mbadala baada ya sili mmoja kukwama barabarani mchana kutwa.

Wenyeji wa jimbo hilo walipiga ripoti kwa maafisa wa kuelekeza magari wakiripoti kuwepo kwa mnyama huyo kwenye barabara ya Highway 37 katika jimbo la Sonoma .

Polisi na wanahabari walipigwa na butwaa walipofika katika eneo hilo na kumuona sili (elephant seal) amekwama barabrani.

Waliwaita maafisa wa huduma ya wanyama pori ambao hawakuwa na maelezo ni vipi mnyama huyo mwenye takriban kilo 500 alipatikana katikati ya barabara kuu.

Licha ya kushtuliwa kupigiwa honi na hata kumwagiwa maji, sili huyo hakubanduka.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Hakuna anayelewa ni vipi mnyama huyo wa baharini mwenye kilo 500 alipatikana barabarani

Mwishowe waliamua kumdunga sindano ya kumlewesha iliwanyanyue wamwondoe barabarani.

Maafisa wa Marine Mammal Center hatimaye walimbeba na kumfanyia vipimo vya siha yake na kugundua kuwa alikuwa ni mjamzito.

Alipelekwa kwenye hifadhi ya wanyama yaP oint Reyes National Seashore ambapo atahudumiwa hadi atakapojifungua kisha arejeshwe baharini.