Uchina kuunda manowari ya pili

Manowari Haki miliki ya picha AP
Image caption Manowari ya kwanza iliyopewa jina Liaoning ilianza kutumiwa na Uchina 2012

Uchina imesema inaunda manowari ya pili yenye uwezo wa kubeba ndege, ikitumia teknolojia kutoka nchini humo.

Meli hiyo ya kivita ya uzani wa tani 50,000 itaundiwa katika bandari ya Dalian, kaskazini mwa nchi hiyo.

Uchina kwa sasa ina manowari moja pekee ya kubeba ndege ambayo iliinunua kutoka Ukraine, ingawa silaha zilizomo ziliwekwa na Uchina.

Taifa hilo linaonekana kuimarisha jeshi lake la wanamaji wakati ambao limehusika katika msururu wa mizozo ya umiliki wa maeneo ya bahari kusini na mashariki.