Ouattara awasamehe wafungwa 3,000 Ivory Coast

Ouattara Haki miliki ya picha
Image caption Bw Ouattara alichaguliwa kuongoza kwa muhula mwingine Oktoba

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amewasamehe zaidi ya wafungwa 3,000 waliokamatwa wakati wa mzozo uliofuatia uchaguzi mkuu miaka mitano iliyopita.

Akitangaza msamaha huo wakati wa hotuba yake ya kuukaribisha mwaka mpya Rais Ouattara amesema kuwa wengi wa wafungwa wataachiliwa mara moja.

Kunao wengine ambao vifungo vyao vitapunguzwa.

Mapigano yalitokea nchini Ivory Coast mwaka 2010 wakati rais Laurent Gbagbo alipokataa kukubali ushindi wa Bw Ouatarra.

Bw Gbagbo kwa sasa anazuiliwa mjini The Hague, Uholanzi akisubiri kesi yake kuanza katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Haki miliki ya picha afp
Image caption Bw Gbagbo anazuiliwa mahakama ya ICC Uholanzi

Bw Ouattara alichaguliwa kuongoza kwa muhula mwezi Oktoba.