Islamic State waendelea kushambulia Ramadi

Ramadi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa Ramadi umeharibiwa sana na mapigano

Wapiganaji wa kundi linalojiita Islamic State (IS) wameendelea kushambulia maeneo yaliyo karibu na mji wa Ramadi wiki moja baada ya jiji hilo kukombolewa na wanajeshi wa Iraq.

Mengi ya mashambulio yanatekelezwa viungani mwa mji huo maeneo ya kaskazini na mashariki, msemaji wa majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani Kanali Steve Warren, ameambia shirika la habari la AFP.

Amesema wanajeshi wa serikali ya Iraq kufikia sasa wamefanikiwa kuzuia mashambulio yote

Mnamo Ijumaa, kundi hilo lilishambulia kambi ya jeshi karibu na mji huo.

Serikali ya Iraq ilisema wiki iliyopita kwamba ilikuwa imefanikiwa kuukomboa mji wa Ramadi ambao ulikuwa umeshikiliwa na IS tangu Mei.

Kanali Warren amesema kufikia sasa Islamic State hawajafanikiwa kuleta pamoja kundi la wapiganaji wanaoweza kuzidi nguvu wanajeshi wa Iraq.