Iran yaitaka Nigeria kumwachilia kiongozi wa Kishia

Zakzaky Haki miliki ya picha AP
Image caption Iran huongozwa na Washia

Iran imeitaka Nigeria kumwachilia huru kiongozi wa Kishia Sheikh Ibrahim al Zakzaky aliyekamatwa baada ya vurugu kutokea kati ya wafuasi wa kundi lake na wanajeshi mwezi uliopita.

Iran imesema itatumia njia zote za kidiplomasia kuhakikisha kiongozi huyo anaachiliwa.

''Tumetumia njia zote kuwaonya Nigeria kuhusiana na kisa hiki. Tunatumai serikali .... itachukua uamuzi bora kuhusiana na suala hili nyeti,'' msemaji wa wizara ya masuala ya ndani Hoseyn Jaber- Ansari ameambia wanahabari katika mji mkuu wa Tehran.

Sheikk al Zakzaky baada ya wanachama wa kundi lake la Islamic Movement of Nigeria (IMN) kukabiliana na wanajeshi kaskazini mwa mji wa Zaria.

Kikundi cha wanaharakati wa kupigania haki za kinadamu limesema karibu watu 300 wa kundi la IMN waliuawa na kuzikwa kwa haraka wakati wa makabiliano hayo.

Jeshi la Nigeria limekanusha madai hayo.

Jeshi hilo limelilaumu kundi hilo, linaloungwa mkono na Iran, kwa kujaribu kumuua mkuu wa majeshi Jenerali Tukur Buratai, madai ambayo kundi hilo limekanusha.

Kwa hivi sasa, Iran imejipata katika mzozo wa kidiplomasia na Saudi Arabia kutokana na mauaji ya kiongozi mashuhuri wa Kishia Sheikh Nimkh Nimr al -Nimr.