Maandamano makubwa kufuatia adhabu ya kifo aliyopewa mhubiri wa madhehebu ya Shia
Huwezi kusikiliza tena

Saud yachukua hatua zaidi dhidi ya Iran

Saud Arabia imetoa kauli kwamba inasitisha safari za anga pamoja na uhusiano wa kibiashara baina yake na nchi ya Iran, na kwamba raia wa Saud watapigwa marufuku kuitembelea nchi hiyo .

Tamko hili limekuja baada ya mafaruku mkubwa ulioko baina ya nchi mbili hizo kufuatia Saud kutoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa mhubiri wa kiislamu wa madhehebu ya Shia, Nimr al Nimr. Hapo kabla Riyadh ilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na Teheran.na hali hii inafuatia kushambuliwa kwa ubalozi wa Saud na waandamanaji waliokuwa na hasira kufuatia taarifa za hukumu hiyo ya kifo.

Naye waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry inaarifiwa amefanya mawasiliano na mawaziri wenziwe wa pande zote mbili katika juhudi za kujaribu kutuliza hali ya mambo.

Mwandishi wa BBC, Regina Mziwanda alizungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa za kitaifa na kimataifa Said Msonga kutoka mijini Dar-Es-Salaam, na nimetaka kufahamu kutoka kwake juu ya Mgogoro huu wa kidiplomasia kuwa unaweza kuathiri vipi uhusiano wa waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni walioko barani Afrika.