Waziri ashtakiwa pesa za Boko Haram Nigeria

Haliru Haki miliki ya picha EFCC
Image caption Bw Haliru alikuwa waziri Julai 2011 hadi Juni 2012

Waziri wa ulinzi wa zamani nchini Nigeria, Bello Haliru Mohammed, ameshtakiwa kutumia vibaya pesa za serikali.

Atatuhumiwa, pamoja na mwanawe Abba Bello Mohammed, kwamba alichukua $1.5m (£1m) zilizopangiwa kutumiwa kununua silaha za kutumiwa na wanajeshi kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo wakati wa utawala wa Rais aliyeondoka madarakani Goodluck Jonathan.

Wawili hao wamekanusha mashtaka hayo.

Waziri huyo wa zamani anadaiwa kuugua, na alifika kortini Abuja akiwa kwenye kiti cha magurudumu Jumanne.

Yeye na mwanawe wanatarajiwa kurejea kortini Alhamisi kwa kikao kuhusu kuachiliwa kwa dhamana.