Afisa wa soka Nigeria auawa kwa risasi

Abubakar Haki miliki ya picha WhatsApp
Image caption Abubakar alikuwa mkuu wa itifaki shirikisho la soka la Nigeria

Afisa wa shirikisho la soka la Nigeria Ibrahim Abubakar amepigwa risasi na kuuawa kwenye nyumba yake mjini Abuja.

Abubakar alikuwa mkuu wa itifaki wa shirikisho la soka nchini humo.

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Nwankwo Kanu, akiandika katika mitandao ya kijamii, amesema amesikitishwa sana na kifo cha Abubakar.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema Abubakar amewaacha mke na watoto watatu. Atazikwa Kaduna, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Afisa wa habari wa timu ya kitaifa Super Eagles, Oluwatoyin Ibitoye amesema mauaji hayo ni ya kusikitisha na kukitaja kisa hicho kuwa cha kutamausha.

Nigeria wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki ya kujiandaa kwa mechi ya kombe la taifa bingwa bara Afrika dhidi ya Angola.

Mechi hiyo itachezewa Pretoria saa 18:00 GMT (Saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki) siku ya Jumatano.

Mchezo huo utakuchezwa bila mashabiki kutokana na ombi la waandalizi wa mechi hiyo.