Obama atokwa na machozi akizungumzia silaha

Huwezi kusikiliza tena

Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayotekeleza ni ya kuwafaa
Haki miliki ya picha Reuters

Hii ni kutokana na ongezeko la watu kushambuliwa kwa risasi nchini humo.

Haki miliki ya picha Reuters

Kiongozi huyo anayemaliza muhula wake wa pili mwaka huu alisema kwa sasa yeye hatafuti kura.

Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwa wakipekua na kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha.

Kwa sasa, takwa hilo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa.

Haki miliki ya picha Getty

Wale hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wanunuzi watarajiwa iwapo wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili.

Haki miliki ya picha AP

Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.