Mwana mfalme George aingia shule ya chekechea

George Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwana mfalme George ana umri wa miaka miwili

Picha mbili zimetolewa zikimuonyesha Mwana mfalme George akiwa shuleni siku ya kwanza baada yake kujiunga na shule ya chekechea.

Mwana mfalme huyo mwenye umri wa miaka miwili amejiunga na shule ya Westacre Montessori, karibu na King's Lynn, eneo la Norfolk.

Alipigwa picha na mamake, Catherine, Binti mfalme Msimamizi wa Cambridge, akisimama mbele ya picha iliyochorwa ukutani nje ya majengo ya shule hiyo ya chekechea.

Shule hiyo iko karibu na nyumba wanamokaa Mwanamfalme William na Binti mfalme Kate eneo la Anmer Hall katika shamba la malkia la Sandringham.

Mwana mfalme George atasomea shule hiyo wazazi wake watakapokuwa wakikaa nyumba hiyo ya Norfolk pekee. Sana, wazazi hao huishi kasri la Kensington.

Haki miliki ya picha Duchess of Cambridge

Shule hiyo hufuata mfumo na maadili ya daktari Mwitaliano Maria Montessori aliyeanzisha mfumo mpya wa kuwafundisha watoto mapema karne ya 20.

Mfumo huo huwaruhusu watoto kuchukua udhibiti wa masomo yao.

Babake mwanamflame George William alikuwa mtu wa hadhi ya juu wa familia ya kifalme Uingereza kwenda shule ya chekechea badala ya kusomea kwenye kasri.