Uwanja wa kisasa wa ndege wafunguliwa Somalia

Somalia Haki miliki ya picha Villapuntland
Image caption Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud ameongoza ufunguzi wa uwanja huo

Serikali ya Somalia imefungua uwanja wa ndege wa kisasa ambao utaweza kupokea ndege za aina yote za kubeba abiria na mizigo.

Uwanja huo ulio mjini Bosaso, umefunguliwa na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud aliyesema ni ufanisi mkubwa kwa taifa hilo.

Uwanja huo umeengwa kwa muda wa miaka miwili unusu na kampuni inayomilikiwa na serikali ya Uchina.

Seikali ya Italia ndiyo iliyofadhili ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa kimataifa wa Bosaso, ambao ndio mkubwa zaidi kujengwa nchini Somalia.

Eneo la mapokezi la uwanja huo limejengwa kwa viwango vya kisasa.

Kuna maafisa wa usalama watakaoshika doria saa 24 kila siku pamoja na maafisa wa uhamiaji watakaokagua wanaoingia na kutoka.

Uwanja huu utatumika sana na ndege za kibiashara, za abiria na unatarajiwa pia kutumiwa na Umoja wa Mataifa.

Utakuwa wa kwanza kufanya kazi usiku nchini somalia.

Mji wa Bosaso ni mji wa bandarini na ndio wa tatu kwa ukubwa nchini Somalia. Unapatikana katika jimbo la Puntland kaskazini mwa Somalia.