Kitabu cha mapenzi kati ya Myahudi na Mpalestina chauza

Image caption Dorit Rabinyan

Kitabu cha mapenzi kati ya raia Myahudi na mwenzake Muislamu wa Palestina kinaongoza kwa mauzo baada ya wizara ya elimu nchini Israel kukataa kukiorodhesha katika mtaala wa elimu shuleni.

Maafisa walihofia kwamba Borderlife kilichotungwa na Dorit Rabinyan kinaweza kuongeza uhusiano wa kimapenzi kati ya raia wa Kiyahudi na wenzao wa Kiarabu.

Lakini hatua hiyo ilizua hisia kali na kukifanya kitabu hicho kununuliwa na wengi.

Uchapishaji ughaibuni pia unaharakishwa na tafsiri yake inajadiliwa nchini Hungury,Uhispania na Brazil.

Ajenti wa Bi Rabinyan amesema kuwa zaidi ya vitabu 5,000 vimeuzwa katika juma moja pekee,vingi vikiuzwa katika soko la Israel huku maduka mengi yakiwa yamemaliza vitabu hivyo.