Washukiwa wa IS wauawa Misri

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Misri

Vikosi vya Usalama nchini Misri vimewapiga risasi washukiwa wawili wa Islamic State baada ya kuvamia hoteli moja kwenye mwambao wa bahari nyekundu ya Hurghada.

Watali 3 kutoka Ulaya walijeruhiwa katika shambulio hilo ,baada ya wanamgambo hao kuingia kwenye hoteli na kuwakabili wageni huku wakipeperusha bendera nyeusi ya IS .

Eneo la tukio hilo lilifungwa kwa uchunguzi.

Ni shambulio la pili katika eneo hilo linalopendwa na watalii hasa nyakati za mapumziko ambapo shughuli za utalii zimedorora tangu kudunguliwa kwa ndege ya Urusi mwezi Novemba mwaka jana na kile ambacho IS ilitaja kuwa ni bomu