Iran:'Hatutaki uhasama uwe m'baya zaidi'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mohammed Javad Zarrif

Waziri wa mambo ya nje wa Iran , Mohammad Javad Zarif, ameuambia Umoja wa Mataifa kwamba nchi yake haitaki uhasama uliopo kwa sasa mashariki ya kati kuwa mbaya zaidi.

Mzozo baina ya Iran na Saudi uliibuka wiki moja iliopita baada ya Ufalme wa Saudia kumuua kiongozi wa madhehebu ya Shia kwa shutuma za ugaidi

Katika barua yake kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon Bwan Zarif aliushutumu utawala wa Riyadh kwa kuunga mkono makundi yenye itikadi kali na kuanzisha vita visivyokuwa na maana nchini Yemen ambako muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unapigana na waasi wa Houthi wa Madhehebu ya Shia.

Kwa upande wake Saudi Arabia inasema serikali ya Iran inajaribu kupata ngome yake nchini Yemen kwa kuwaunga mkono Wahuthi.

Baraza la Utendaji la Ghuba linatarajia kukutana mjini Riyadh leo kujadili mzozo huo.