Cameron:Nitashikilia wadhfa wangu 'nikishindwa'

Haki miliki ya picha EPA
Image caption David Cameron

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa ataendelea na wadhfa wake hata iwapo atapoteza kura ya maamuzi kuhusu uanachama wa Muungano wa Ulaya.

Cameron amemwambia mwandishi wa BBC Andrew Marr kwamba hafikiria kuondoka katika muungano wa Ulaya ndio suluhu,lakini serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inasalia katika muungano huo,iwapo Waingereza watapiga kura ya kuondoka.

Pia amesema kwamba ana matumaini makubaliano yataafikiwa ifikiapo mwezi Februari kuhusu mabadiliko ya Muungano huo anayopigania kabla ya kura hiyo kufanyika.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Muungano wa Ulaya

Kura hiyo ya maamuzi iliahidiwa kufanyika mwisho wa 2017.

Moja ya maswala yake muhimu ambayo anapigania ni kuzuiwa kwa miaka minne faida za wafanyikazi wahamiaji wa muungano huo ,hatua ambayo imepingwa na wenzake wa muungano huo,lakini Cameron amesema kuwa ataendelea kusukuma wazo hilo hadi pale suluhu m'badala itakapopendekezwa.