HRW lawashtumu waasi wa Houthi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waasi wa Houthi

Shirika la haki za kibinadamu lenye makao yake nchini Marekani Human Rights Watch limeshutumu kundi la waasi wa Houth nchini Yemen kwa vitendo vyake vya utesaji wa kinyama na kuwashikilia wapinzani wao katika mji mkuu wa Yemen wa Sanaa.

Image caption Shirika la haki za kibinaadamu la Human Rights Watch

Shirika hilo limesema lilifanya kipindi maalumu na kuwatazama watu 35 majira ya kiangazi mwaka jana ambapo watu hao wengi wao wangali wako kizuizini. Limeongeza kuwa shirika jingine la kisheria la nchini Yemen linafanyia kazi wafungwa wengine waliopo kizuzini zaidi ya mia nane na watu wengine waliopotea.

Kundi la Houthi linaushirikilia mji wa mkuu wa Yemen Sanaa kwa zaidi ya mwaka sasa licha ya juhudi za majeshi ya serikali na washirika wao wa Saudi Arabia kupambana kuwaondosha.