Bunge la Misri lafanya kikao cha kwanza

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bunge la Misri kufanya kikao chake cha kwanza

Bunge la Misri linafanya kikao chake cha kwanza cha wazi ikiwa ni miaka mitatu tangu bunge hilo lililokuwa chini ya chama cha kiislam kuvunjwa na mahakama kwa sababu za ujanja wa kisheria.

Kikao cha leo kinatarajiwa kumchagua spika wa bunge.

Kikao hicho kitakuwa na siku kumi na tano kufanya mabadiliko ya kisheria kadhaa ambazo zimewasilishwa na rais wa Misri jenerali wa jeshi Abdel Fattah el-sisi aliyeipindua serikali iliyochaguliwa na wananchi iliyokuwa chini ya chama cha Muslim Brotherhood na rais Mohamed Morsi mwaka 2013.

Bunge la sasa linahodhiwa na wafuasi wa rais Al asisi.