Kitabu kipya cha Papa kuchapishwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa Francis

Makao makuu ya kanisa katoliki mjini Vatican yamefichua maelezo kuhusu kitabu kipya cha papa Francis "the name of God is Mercy" jina la Mungu ni rehema, kitakachochapishwa kote duniani kwa muda wa siku mbili zijazo.

Maandishi ya kitabu hicho yanatokana na mahojiano kati ya papa na mwanahabari, ambapo anaangazia mada ya rehema, na umuhimu wa kuwa na rehema kwa watu waliotengwa katika jamii.

Papa pia anaangazia jinsi ambavyo huwa anaomba msamaha wakati wa kutubu.