Mgombea ataka kura kuhesabiwa upya CAR

Haki miliki ya picha
Image caption Mgombea Martin Ziguele

Mgombea mkuu katika uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ametaka kura kutoka kwa duru wa kwanza kuhesabiwa kwa mikono kufuatia madai ya kuwepo udanganyifu .

Martin Ziguele, ambaye ni waziri mkuu wa zamani ambaye alichukua nafasi ya nne kati ya wagombea 30 kwenye kura zilizopigwa tarehe 30 mwezi Desemba, alipanga kwenda kwa mahakama ya kikatiba kutaka kura hizo zihesabiwe kwa mikoni.

Chama chake cha Movement for the Liberation of the Central African People (MLPC) kinawalaumu maafisa wa uchaguzi kwa kuvuruga matokeo kutoka sehemu tofauti za nchi na kufanya vigumu kufuatilia matokeo hayo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndio uchaguzi wa kwanza tangu ghasia zianze mwaka 2013

Matokeo ya kwanza yalionyesha kuwa hakukuwa na mshindi, hatua ambayo italazimisha kufanyika kwa duru nyingine kati ya mawaziri waku wa zamani - Georges Dologuele na Faustin Archange Touadera.

Uchaguzi huo ndio wa kwanza tangu ghasia zianze chini ya misingi ya kidini mwaka 2013 kati ya makundi ya wakiristo na waislamu. Zaidi ya robo ya raia wa nchi hiyo wamelazimishwa kuhama makwao.