Binti Cristina wa uhispania ashtakiwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Binti wa kifalme, Cristina wa uhispania

Binti wa kifalme Cristina wa uhispania ambaye yuko katika nafasi ya sita katika urithi nchini humo ameshtakiwa kwa ufisadi.

Kesi yake inahusu shughuli za kibiashara za mmewe, Inaki Urdangarin. Analaumiwa kwa matumizi mabaya ya zaidi ya dola millioni sita kutoka shirika moja lisilolenga faida.

Aidha analaumiwa kwa kushindwa kuijulisha halmashauri ya kukusanya ushuru kuhusu, mapato ya shirika hilo. Wawili hao wamekana kufanya lolote baya.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Cristina anakabiliwa na kifungo cha miaka minane jela ikiwa atapatikana na hatia

Princes Cristina ambaye ni dadake mfalme Felipe, ndiye mtu wa kwanza wa familia ya kifalme nchini uhispania kufunguliwa mashtaka tangu ufalme huo urejeshwe miaka ya sabini.

Princes Cristina aliye na miaka 50 anakabiliwa na kifungo cha miaka minane jela ikiwa atapatikana na hatia na jopo la majaji watatu.

Kesi hiyo inatajwa kuwa aibu kubwa kwa familia ya kifalme.