Pistorius anuia kubadilisha hukumu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Oscar Pistorius

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ametuma ombi kwenda kwa mahakama ya kikatiba nchini humo la kutaka aruhusiwe kubadili uamuzi katika kesi ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Mahakama ya rufaa ilibadili hukumu ya awali ya kumuua Bi Steenkamp kutoka kuua bila kukusudia hadi kuua.

Lakini mawakili wake wanasema kuwa mahakama ilifanya makosa. Pistorius anakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 15 ikiwa atashindwa kubadili uamuzi huo wa mahakama ya rufaa.