Ndovu wapungua kwa kasi Tanzania

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Matokeo yanaonyesha kuwa ndovu walipungua kutoka 109,000 mwaka 2009 hadi ndovu 51,000 mwaka 2015

Matokeo kutokana na shughuli kubwa zaidi ya kuhesabu ndovu katika historia ambayo ilimazika juzi nchini Tanzania, yanaonyesha kuwa kuna kupungua kwa kasi kwa idadi ya ndovu kutoka ndovu 109,000 mwaka 2009 hadi ndovu 51,000 mwaka 2015.

Shughuli hiyo ni mpango ulidhaminiwa na tajiri raia wa marekani Paul Allen ulio na nia ya kuelewa zaidi idadi ya ndovu kote barani Afrika.

Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika zaidi na uwindaji haramu kufuatia kuwepo kwa biashara haramu ya pembe za ndovu nchini China.