Wafungwa ni mashabiki wakubwa wa Ghana

Haki miliki ya picha .
Image caption Wafungwa wa Guantanamo wanaishabikia Ghana

Sasa imebainika kuwa wafungwa katika gereza la jeshi la marekani la Guantanamo Bay ni wafuasi sugu wa timu ya taifa ya Ghana, the Black Stars.

Hii ni kwa mujibu wa waliokuwa wafungwa katika gereza hilo raia wa Yemen ambao waliachiliwa hivi majuzi na kupelekwa nchini Ghana.

Wakizunguzma na kituo cha Radio cha Uniiq FM walisema kwa wengi wa wafungwa walikuwa ni mashabiki wa Black Stars wakati wa mechi za kombe la dunia za mwaka 2010.

Walipoulizwa ni kwa nini wakaamua kuwa mashabiki wa Ghana?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waliishabikia Ghana kwa sababu waliishinda Marekani

Walisema kuwa Ghana ndio waliiondoa marekani kutoka kwa kinyanganyiro cha kombe la dunia katika kundi la mwisho la timu 16.

Mshambuliaja Asamoah Gyan ambaye wawili hao walisema walimshabikia zaidi, alizima matumaini ya kikosi cha marekani dakika za mwisho mwisho.

Wakati Ghana iliishinda marekani tulifurahi sana. Tulisherehekea. Pia tuliwaambia walinzi kuwa tumeshinda , Mahmoud Omar Bin Atef ambaye alizuiliwa kwa miaka kumi bila mashtaka alikiambaia kituo hicho cha Radio.