Iran yashikilia boti za Marekani

Haki miliki ya picha AP

Boti mbili za doria za Marekani zikiwa na wafanyakazi 10 zimekamatwa nchini Iran.

Maafisa wa Marekani wamesema boti hizo zilikuwa katika mazoezi kati ya Kuwait na Bahrain kwenye eneo la Ghuba, baada ya moja wapo kupata matatizo ya kiufundi na kupoteza mwelekeo hadi katika maji ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani John Kery amewasiliana na mwenziye wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye amemhakikishia kwamba wanamaji wa boti hiyo watarudishwa mara moja.

Shirika la Habari la Iran limesema boti hizo zimeingia katika maji ya Iran kinyume cha sheria.