Makanisa yaikosoa serikali Kenya

Image caption Makanisa yanasema hatua hiyo ina lengo la kuzuia kuongezeka kwa makanisa.

Makanisa nchini kenya yameilaumu serikali kwa mapendekezo yake ya kubuni sheria ambazo zitafanya vigumu kwa makasi hayo kutekeleza kazi zao.

Chama cha makanisa nchini kenya kinasema kuwa hatua hiyo ina lengo la kuzuia kuongezeka kwa makanisa.

Lakini kiongozi mmoja mashuhuri wa kianglikana amekaribisha mapendekezo hayo ya serikali akiyataja kama njia bora ya kuzuia makanisa kutumiwa kama biashara.

Image caption Makanisa yanasema hatua hiyo ina lengo la kuzuia kuongezeka kwa makanisa.

Mapendekezo hayo yanazitaka dini zote kujiandikisha na wahudu kuwa na vibali kutoka kwa polisi.

Wakristo ndio wengi zaidi nchini Kenya wakifuatiwa na waislamu. Baraza kuu la waislamu nchini kenya nalo pia limepinga mapendekezo hayo likionya kuwa yatakiuka uhuru wa kuabudu.

Kanisa katoliki ambalo ndilo lenye wafuasi wengi zaidi nchini Kenya na ambalo rais Uhuru Kenyatta anahudhuria bado halijatamka lolote kuhusu mapendekezo hayo.